Thursday, January 21, 2010

Karibuni Barazani

Habari zenu ndugu zangu,

Ni matumaini yangu kuwa mnaendelea vyema na shughuli zenu za kila siku,tunashukuru mungu kwa hilo.Tumenzisha baraza hili ili kupata fursa za kutuwezesha kupashana habari,fikra,mawazo,na pia kusalimia na kudumisha ile mila yetu ya ukaribu uliotenganishwa na umbali wa kijiografia kwa sababu mbalimbali za kimaisha.

Wazo la kuanzisha thread hii lilitokana na majadiliano baina ya wajubaz wawili,Ally-kebby na Yassin (Dogo) Kambula, na lilifikishwa kwa Hadji nae akaafiki,hivyo nimechukua hatua ya kuanzisha,ni matumaini yetu kuwa tutaweza kutumia platform hii kudumisha ile jadi yetu,nafahamu kuna mabadiliko ya kimaendeleo na kifikra yanatokea miongoni mwetu,tujitahidi kuweza kutumia hii blog kwa ufanisi na kutimiza lengo.

Bado hiko katika hatua za mwanzo,kila moja ana haki ya kutoa mchango,mawazo na mbinu mbalimbali hili kuiboresha na kuipendezesha blog yetu ya wajubazz.

Jamvi liwazi karibuni sana.

Moderator wa muda
Ally-Kebby

No comments:

Post a Comment